TANGAZO


Thursday, June 7, 2012

TBL yatoa vifaa vya usafi vya sh. milioni 12 Ilala



Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 12 kwa ajili ya Manispaa ya Ilala, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, Dar es Salaam jana.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, akiendesha moja kati ya matolori yaliyotolewa msaada na TBL kwa Manispaa ya Ilala. Kulia ni Steve Kilindo wa TBL.

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mushi (kushoto) na Steve Kilindo wa TBL, wakifagia ikiwa ni ndio uzinduzi rasmi wa maadhimisho hayo karibu na Soko la Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam.

 Watumishi wa Manispaa ya Ilala na Wafanyakazi wa TBL, wakifanya usafi kwa pamoja kwenye mtaa wa Muheza, Kariakoo jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi huo.

 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo (katikati), akizoa taka wakati wa kampeni hiyo ya usafi wa mazingira. (Picha zote kwa hisani ya Francis Dande.blogspot)

No comments:

Post a Comment