TANGAZO


Friday, June 1, 2012

Stars wajifua jijini Abidjan kuwakabili Ivory Coast


Wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakiongozwa na mwalimu wao msaidizi Mash (mbele kulia), kupasha kwa ajili ya kujiweka sawa kwa mazoezi ya kuikabili timu ya Taifa ya Ivory Coast, jijini Abidjan kesho kuwania nafasi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.


Wachezaji wa Stars wakiruka wakati wakijifua kwa ajili ya kujiweka tayari kuwakabili Ivory Coast kesho kwa ajili ya kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia, 2014.


Wachezaji wa timu ya Soka ya Taifa ‘Kilimanjaro Taifa Stars’ wakijifua kwenye Uwanja wa wa kituo cha Michezo mjini Abidjan juzi kujiandaa na mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast inayotarajiwa kufayika kesho, Jumamosi Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny. 

Kocha wa timu ya Soka ya Taifa ya ‘Kilimanjaro Taifa Stars’, Kim Poulsen akiwapa mazoezi ya viungo wachezaji wa timu hiyo kwenye uwanja wa kituo cha Michezo mjini Abidjan jana kujiandaa na mchezo wa mchujo wa kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast. Mechi itakayopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny. (Picha zote kwa hisani ya Executive Solution Ltd)

No comments:

Post a Comment