TANGAZO


Thursday, June 21, 2012

Serengeti Breweries yazindua uvunaji maji ya Mvua Iringa

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akizindua rasmi mradi wa uvunaji maji ya mvua uliopo Hospitali ya Wilaya ya Iringa Frelimo mjini hapa leo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 50 na unatarajiwa kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo zaidi ya 100,000. Wengine kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi, Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu, V. Mushi.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba (kushoto), akimshukuru Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda kutokana na Kampuni yake kufadhili mradi huo muhimu wa maji hospitalini hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba, akifungua maji kutoka katika tanki moja wapo la mradi huo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba, akimtwisha ndoo ya maji Augusta Mtemi ambaye ni Diwani wa viti maalum Iringa, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi huo.

 Diwani Augusta Mtemi akifurahia baada ya kumtwisha ndoo ya maji diwani huyo, wakati wa uzinduzi huo.

 Matanki ya maji makubwa yaliyowekwa ardhini ya mradi huo, hospitalini hapo.

 Tanki litakalo tumika kusambaza maji katika mradi huo.

Hopspitali ya Frelimo iliyopo Manipaa ya Iringa ambayo mradi huo umezindulia na kuwa moja itafaidika na maji ya mradi huo. (Picha zote na Mroky Mrocky)

No comments:

Post a Comment