TANGAZO


Friday, June 1, 2012

Rodgers atoa ahadi kwa Liverpool

Brendan Rodgers
Amesema atapambana "kufa kupona" ili kuiwezesha Liverpool kupata ubingwa
Meneja mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers, ameahidi atafanya juhudi za "kufa kupona" katika kuiletea ubingwa klabu hiyo ya uwanja wa Anfield.
Rodgers, mwenye umri wa miaka 39, alithibitishwa kama mrithi wa Kenny Dalglish baada ya klabu yake ya Swansea kukubali kuchukua senti za fidia katika kumpoteza meneja huyo.
"Ninatoa ahadi za kupambana kufa kupona maishani kwa niaba ya watu wa mji huu," alielezea raia huyo wa Ireland ya Kaskazini.
"Pengine sasa hivi hatujajiandaa kwa ubingwa, lakini utaratibu wa kufanya hivyo unaanza leo."
Inafahamika Swansea wamekubali kitita cha pauni milioni 7 kumruhusu Rodgers kuondoka, na vile vile wasaidizi wake kocha Colin Pascoe, Chris Davies anayehusika na ubora wa mchezo, na Glen Driscoll, mshauri wa klabu kuhusiana na ubora wa mchezo, na waliopata mkataba wa miaka mitatu.
Liverpool wametwaa ubingwa wa ligi mara 18 katika historia yao, na mara ya mwisho walipata ubingwa msimu wa 1989-90.
"Huu ni muda mrefu uliopita na ndio maana kazi hii ni kivutio," alielezea kocha huyo wa zamani wa timu za Watford na Reading vilevile.
"Kilichonivutia mimi ni historia ya klabu na mashaka iliyoyapata. Ni miaka 20 sasa tangu walipopata ubingwa."
"Hii ni klabu ambayo ukipata ufanisi, basi utakuwa hapa kwa miaka mingi.
"Hii ndio sababu ya kufika hapa. Bila shaka yote yanahusiana na matokeo na ufanisi wa timu. Of course that is about results and the progress of the team.
"Ni fahari kubwa kwangu. Ninahisi nimebarikiwa kuipata nafasi hii kuisimamia klabu.".
Mashabiki wa Liverpool bado hawana uhakika kumpokea vipi Rodgers, lakini meneja huyo amesema ataweza kuwashawishi mashabiki wote wa uwanja wa Anfield kwamba ataweza kukimudu kibarua hicho.
"Natumaini baada ya muda wataweza kunikubali na kuniheshimu," alielezea.
"Ni klabu maalum. Nina hamu sana ya kuhamia na kuishi katika mji huu."

No comments:

Post a Comment