Mmoja wa Wamiliki wa Shamba la Mboga katika kijiji cha Chikopelo, Alon Hoven kimwonesha Rais Jakaya Mrisho Kikwete, baadhi ya mazao yanayozalishwa kwa kutumia mbegu bora pamoja na teknolojia ya umwagiliaji wa matone wakati Rais alipotembelea shamba hilo katika kijiji cha Chikopelo, wilayani Bahi, mkoani Dodoma leo asubuhi. Shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mia moja linamilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade chini ya Dunstan Mrutu na Alon Hoven raia wa Israel.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Rais Kikwete alisifu juhudi za
wawekezaji hao kwa kutumia mbinu za kisasa za kilimo na kuwaasa wanakijiji wa
Chikopelo kujifunza mbinu bora za kilimo hicho cha mboga ili waweze kupata
ufanisi na kuboresha maisha yao. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaonya viongozi
wa kijiji cha Chikopelo kutoendelea kuuza ardhi yote kwa wawekezaji na badala
yake kutunza na kuilinda kwaajili ya kizazi kijacho.
Awali katika salamu zao kwa Rais,bBwana Dunstan Mrutu na mmiliki
mwenzake, Alon Hoven mbali na kutoa ajira kwa wanakijiji hao waliahidi
kushirikiana nao katika kujifunza mbinu bora za kilimo na kuwawezesha kuzalisha
mazao bora na mengi.
No comments:
Post a Comment