Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao leo Juni 4, 2012, katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha. Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kesho, ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao leo Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha na kufanya nao mazungumzo. Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kesho ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao leo Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha. Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kesho ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao. (Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment