Mkazi wa Kata ya Tanga, mjini Songea, Kamanda Nico, akimsalimia Nape katika mapokezi hayo.
Nape akimtuza kijana wa Madrasaatul Nabai ya Masigira, baada ya kijana huyo kuomba dua alipowasili mjini Songea.
Nape akizindua mradi mabanda 119 ya biashara eneo la Mshengano, Songea. Vibanda hivyo vya CCM vimejengwa na Chama Cha Mapinduzi kwa sh. milioni 206.
Nape akifungua Shina la wakereketwa wa CCM, wafanyabiashara kwenye mabanda ya Chama, Kata ya Mshengano, Songea jana.
Msafara wa pikipiki ukiongoza msafara wa Nape kwenda Uwanja wa Majimaji, mjini Songea jana.
Nape akishiriki kucheza ngoma, baada ya kuwasili Uwanja wa Majimaji, mjini Songe jana.
Nape akisaidia kupiga ngoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea.
Nape akisalimia wananchi, alipowasili Uwanja wa Majimaji, mjini Songe kuhutubia mkutano wa hadhara.
Nape akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia wananchi, wanachama na wakereketwa wa Chama hicho Uwanja wa Majimaji, mjini Songea jana.
Akina mama wakigaragara chini mbele ya Nape (jukwaani), baada ya kuingiwa na kupandwa na hamasa wakati Nape akitoa hotuba yake.
Nape akipita kwenye kanga zilizotandikwa na akina mama waliovutiwa na hotuba yake.
Nape akiondoka Uwanja wa Majimaji baada ya mkutano huo wa hadhara mjini Songea jana. (Picha zote na Bashir Nkoromo, Songea)
No comments:
Post a Comment