TANGAZO


Saturday, June 2, 2012

Rais Kikwete akutana na mmiliki wa timu ya Portsmouth ya Uingereza


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akimkaribisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dk. Sulaiman Al Fahim, wakati walipokutana leo, Jumamosi, Juni 2, 2012, Ikulu jijini Dar es Salaam. Dk. Al Fahim ni Mwenyekiti wa zamani na mmiliki mwenza wa Klabu ya soka ya Portsmouth ya Uingereza, yuko nchini kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika uchumi wa Tanzania. Dk. Al Fahim ndiye aliyeongoza mazungumzo na kununuliwa kwa klabu bingwa ya Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester City na Kampuni ya Arabuni. (Picha na Fredy Maro).

Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika mzungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dk. Sulaiman Al Fahim, Ikulu leo.

Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dk. Sulaiman Al Fahim mara baada ya  mazungumzo yao, Ikulu jijini leo.

No comments:

Post a Comment