Nape Nnauye akagua ujenzi wa Hospitali ya Rufani, Singida
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa Chama hicho, Mkoa wa Singida baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Juni Mosi, 2012.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Liana Hassan (wapili kulia), akionesha ramani ya jengo la Utawala la Hospitali ya rufani ya Mkoa wa Singida ambayo ujenzi wake unaendelea. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida, Jerome Alute.
Nape na ujumbe wake wakiangalia jengo la Wazazi la Hospitali ya Rufani ya Singida baada ya kufika kwenye jengo hilo leo.
Nape Nnauye, akikagua ndani ya majengo ya Hospitali ya Rufani ya Singida, baada ya kufika hospitalini hapo kuangalia shughuli mbalimbali za ujenzi.
Ofisa Tawala wa Mkoa wa Singida, Liana Hassan (kushoto), akimpatia maelezo Nape Nnauye, kuhusu ujenzi wa Hospitali hiyo ulipofika kuangalia shughuli mbalimbali. Kulia ni Alute.
Nape Nnauye, akizunguka nje ya jengo la Hospitali ya Rufani ya Singida, kuangalia mandhari yake leo.
No comments:
Post a Comment