Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News na Habri Leo, yanayomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Standard Newspaper, Athuman Hamis, ambaye alipata ajali iliyomsababishia baadhi ya viungo vyake kutokufanyakazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kukosa huduma alizokuwa akizipata kutoka kwa taasisi mbalimbali zilizokuwa zikimsaidia hapo awali, ikiwemo mwajiri wake, hadi kulazimika kuomba msaada kwa wasamaria wema nchini, ili aweze kujikimu kimaisha. Kulia ni Msaidizi wake wa huduma za matibabu (Nurse), Elizabeth Richard.
Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News na Habri Leo, yanayomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Standard Newspaper, Athuman Hamis, ambaye alipata ajali iliyomsababishia baadhi ya viungo vyake kutokufanyakazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kukosa huduma alizokuwa akizipata kutoka kwa taasisi mbalimbali zilizokuwa zikimsaidia hapo awali, ikiwemo mwajiri wake, hadi kulazimika kuomba msaada kwa wasamaria wema nchini, ili aweze kujikimu kimaisha. Kushoto ni Msaidizi wake wa huduma mbalimbali Razak Mohamed.
Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News na Habri Leo, yanayomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Standard Newspaper, Athuman Hamis, ambaye alipata ajali iliyomsababishia baadhi ya viungo vyake kutokufanyakazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kukosa huduma alizokuwa akizipata kutoka kwa taasisi mbalimbali zilizokuwa zikimsaidia hapo awali, ikiwemo mwajiri wake, hadi kulazimika kuomba msaada kwa wasamaria wema nchini, ili aweze kujikimu kimaisha. Kulia ni Msaidizi wake wa huduma za matibabu (Nurse), Elizabeth Richard na kushoto ni msaidizi wake wa huduma mbalimbali, Razak Mohamed. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
ATHUMAN HAMIS WA DAILY/SUNDAY NEWS, AOMBA MSAADA
Na mwandishi wetu,
5 June, 2012.
MPIGAPICHA Mkuu wa Shirika la Magazeti ya Serikali la Tanzania Standard Newspapers, linalotoa magazeti ya Daily/Sunday News na Habri Leo, Athumani Hamisi, anaomba msaada kwa Makampuni, Mashirika, Wizara, Shirika la nyumba la Taifa (NHC), Watu binafsi, Serikali na Taasisi yoyote watakayoguswa na kilio chake, kumsaidia kwa njia yoyote ili aweze kujikimu kimaisha kutokana na hali zake kumwendea kombo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo, Hamis, alisema kwamba baada ya kuona hali yake ya kimaisha inazidi kuwa ngumu, amelazimika kujitokeza hadharani ili kutafuta msaada utakoweza kuokoa maisha yake kutokana na kuwa na kipato duni na hali za ulemavu wa viungo alioupata kutokana na ajali ya gari iliyompata zaidi ya miaka 7 sasa.
Hali hiyo, imekuja baada ya taasisi zilizokuwa zimejitolea kumsaidia hapo mwanzo, mara tu baada ya kupata ajali amabapo alisafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini kutibiwa kutokana na ajali hiyo, ambayo ilimsababishia viungo vyake kutokufanyakazi, ikiwemo uti wa mgongo ambao hadi sasa unamsumbua kujitoa, baada ya kumhudumia hata pale aliporejea nchini.
Alisema kuwa hali imekuwa mbaya zaidi baada ya hata yule msaidizi wake aliyekuja naye kutoka Afrika Kusini, akimhudumia kuondoka kutokana na taasisi iliyokuwa ikimlipa kuacha kuanya hivyo na yeye pia kukosa huduma za kiafya pamoja na matumizi ya kujikimu kimaisha pamoja na familia yake, yenye watoto watatu wanaosoma shule za kulipia.
"Sasa ninaishi Kimungumungu tu kwa kweli sina msaada wowote ninaoupata, hata mwajiri wangu hela anayonilipa haitoshi hata kuwalipa hawa wasaidizi wangu siuze kula, watoto kusoma, matibabu na mambo mengine ya kimaisha. Kwakweli ninaishi kwa tabu sana hivi sasa namebaki nikisaidiwa na wale marafiki wangu wa kweli tu, hakuna kingine ninachokipata zaidi ya chakula changu," alisema Hamis.
Hamis, aliyepata ajali hiyo, Septemba 12 mwaka 2008 na kumfanya awe mlemavu wa viungo na kuapata ugonjwa wa uti wa mgongo, alisema kuwa hata nyumba anayoishi, tayari ameshapewa notisi na kumalizika muda wake ambayo inamtaka kuhama kutokana na kodi iliyokuwa ikilipwa na mwajiri wake sasa kutokulipwa tena.
Akielezea hali ya maisha yake kijumla, alisema kamwe hakufikiria ulemavu uliompata ambao umemfanya awe ombaomba kwamba siku moja atakuwa hali kama hiyo aliyonayo na kumshukuru Mungu hata hivyo kutoakana na bado kuwa yuko hai.
Alisema kuwa hivi sasa amekuwa akijaribu kupiga simu, kuwapigia baadhi ya viongozi wa taasisi zilizokuwa zikimsaidia pamoja na kutuma meseji, lakini bila hata simu hizo pamoja na meseji kujibiwa.
"Sio siri hali yangu ni mbaya sana kiuchumi ndugu wote wamenikimbia waliobaki ni marafiki wa kweli wameniingiza kwenye familia zao", alisema Hamisi
"Nina watoto watatu wakwanza anamaliza darasa la saba mwaka huu wapili anasoma darasa la nne anaishi na bibi yake na watatu anasoma darasa la pili hawa wote wanasoma shule za kulipia wate nawalipia 200,000 kila mmoja kwa tem jumla ni 400,000 hizo shule zina tem nne kwa mwaka gharama za chakula, vifaa vya wanafunzi kwamwezi inafika 750,000 mpaka 900,000kwa mwezi", alisema.
Alisema hana uwezo wa kulipa nyumba kwa gharama zozote zile anawaomba watanzania watakaoguswa waweze kumsaidia, kubwa ni nyumba ushauri wa madaktali ni kwamba nisiishi mbali na mazingira ya Hospitali kulingana na hali yangu.
No comments:
Post a Comment