TANGAZO


Sunday, June 24, 2012

Mbunge Zungu aikabidhi sh. 4m Shule ya Msingi Upanga, azungumza na wakazi Upanga Mashariki

Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasila, Kata ya Upanga Mashariki, Rukia Riyami, akizungumza katika mkutano wa wakazi wa Kata hiyo, uliofanyika katika Shule ya Msingi ya Upanga jijini Dar es Salaam leo, wakati Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' (kushoto), alipofika kwenye eneo hilo kuzungumza na wakazi wa kata hiyo, kuwasilisha ripoti ya Jimbo na kukabidhi cheki ya sh. milioni 4 kwa shule hiyo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akizunguma na wakazi wa Upanga Mashariki katika mkutano kuwasilisha ripoti ya jimbo na kukabidhi cheki ya sh. milioni 4 kwa Shule ya Msingi Upanga kwa ajili ya shughuli ya kuweka umeme shuleni hapo, jijini leo. Kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasila, Kata ya Upanga Mashariki, Rukia Riyami na kushoto ni Afisa Tarafa ya Kariakoo, Mathiasy Muyenjwa.

Baadhi ya wakazi wa Upanga Mashariki wakiwa kwenye mkutano wao huo, shuleni hapo leo.

Baadhi ya wakazi hao, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye mkutano wao huo, shuleni hapo.

Wakazi wa Upanga Mashariki, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi yao kwenye mkutano wao huo. 

Mkazi wa Upanga Mashariki, Noor Mohamed, akitoa duku duku lake mbele ya mbunge Zungu wakati wa mkutano huo ambapo alimtaka awe anafika mara kwa mara kwenye mitaa yao hiyo na kujibiwa na Mbunge Zungu kuwa mara kwa mara huwa kwenye eneo hilo kwa shughuli mbalimbali lakini hawajabahatika kuonana tu.

Mkazi Fakuruddin Taibali, akitoa maelezo ya hali ilivyo ya shule hiyo ya Upanga pamoja na kuahidi kuisaidia katika suala hilo la umeme shuleni hapo.

Mbunge Mussa Azzan Zungu, Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasila, Kata ya Upanga Mashariki, Rukia Riyami na Mwenyekiti wa mtaa wa Kitonga Marco Rweyimamu (kulia), wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wakazi hao kwenye mkutano huo.

Mkazi Ferdinand Swai, akitoa hoja za kulitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuwauzia nyumba wanazoishi, kwakuwa wameshaishi kwa muda mrefu kwenye nyumba hizo na kuwa Serikali iliahidi nyumba hizo wangeliuziwa wao kwanza.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maktaba, Anna Mshana (kushoto) na wa Upanga, Paschazia Kinyondo, wakiteta jambo kwenye mkutano huo.


Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Upanga, Paschazia Kinyondo hundi ya sh. milioni 4, zilizotoka kwenye mfuko wa jimbo kwa ajili ya shughuli ya kuweka umeme shuleni hapo, wakati wa mkutano wa wakazi wa Kata hiyo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasila, Rukia Riyami na Afisa Mtendaji wa mtaa Kibasila/Kitonga, Dominica Mwacha.


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Upanga, Paschazia Kinyondo, akito shukurani kwa Mbunge Zungu pamoja na wakazi hao kwa kujitolea kuisadia shule hiyo sambamba na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akijibu baadhi ya hoja hizo, zilizowasilishwa kwake na wakazi hao kwanza kabla kwa mara nyingine tena kusikiliza hoja nyingine kutoka kwao.

Baadhi ya wakazi hao, wakifurahia majibu ya hoja mbalmbali yaliyokuwa yakitolewa na Mbunge, Zungu wakati wa mkutano wao huo.

Diwani wa Kata ya Upanga Mashariki, Sultan Salim, akizungumza na wakazi hao, wakati alipokuwa akifafanua na kujibu hoja mbalimbali zilizoelekezwa kwake na baadhi ya wakazi hao kwenye mkutano huo leo. Kulia ni Mbunge Mussa Zungu, akisikiliza majibu hayo.

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Upanga Mashariki wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Diwani wao, Sultan Salim katika mkutano huo, uliohudhuriwa na Mbunge Mussa Azzan Zungu.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kitonga, Kata ya Upanga Mashariki, Marco Rweyimamu, akitoa ufafanuzi wa suala la kuuziwa nyumba kwa wakazi hao, wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' na katikati ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasila katani hapo, Rukia Riyami.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akitoa ufafanuzi na kujibu hoja za wakazi hao kabla ya kuhitimisha mkutano wake na wakazi hao wa Upanga jijini leo. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Upanga Mashariki, Sultan Salim, Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasila katani hapo, Rukia Riyami (kulia) na Afisa Tarafa ya Kariakoo, Mathiasy Muyenjwa.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akisindikizwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Ilala, Alya Riayami na Diwani wa Kata ya Upanga Mashariki, Sultan Salim (nyuma), mara baada ya kumaliza kuzungumza na wakazi hao, Shule ya Msingi ya Upanga jijini Dar es Salaam leo. 

No comments:

Post a Comment