Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, akinywa maji safi ya bomba kwenye kisima ambacho kimegharimu zaidi ya Sh. milioni 6.5, alichokabidhiwa na viongozi wa Lions Club ya Dar es Salaam, Mizizima kwa ajili ya Shule za Msingi za Minazi mirefu na Airwing, katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Minazi mirefu Dar es Salaam jana. Silaa alikuwa mgeni rasmi. Kushoto ni Gavana wa Lions Club Internation Tanzania na Uganda, Satish Sherma.
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akifungua moja ya bomba la maji ya kisima walichokabidhiwa na wahisani hao katika Shule ya Msingi ya Airwing Kipawa. Diwani Kaluwa ndiye aliyefanikisha mpango wa upatikanaji wa visima hivyo kupitia Lions Club.
Gavana wa Lions Club Internation Tanzania na Uganda, Satish Sherma, akitoa hotuba fupi kabla ya kukabidhi visima hivyo.
Gavana wa Lions Club Internation Tanzania na Uganda, Satish Sherma, akimvalisha beji ya Lions Club, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa wakati wa makabidhiano ya visima hivyo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZALluFVI1Z17Y3Dygk9vzfeLFB2MXdVFp98mOz_wcCFBbHlNuzwSKoy7SBPl42n21cH1ts6flrwONu9YkbLpeDpk4CjyKbj_6K-QF3BKfWcI2xuHyOaQXXD8piYx35f4VfmstH0JXp0Q/s640/akiteja+jambo.jpg)
Wanafunzi wa Shule za Minazi Mirefu na Airwing wakipiga makofi wakati wa kukabidhiwa visima hivyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Minazi Mirefu, Daniel Mwamakula (kulia), akitoa neno la shukurani kwa wahisani hao na wageni waalikwa.
No comments:
Post a Comment