TANGAZO


Sunday, June 17, 2012

Mbunge Dewji akabidhi pikipiki 10 na Cement mifuko 25 Singida

Jengo la Kanisa la Pentekoste la kijiji cha Ititi jimbo la Singida mjini, ambalo Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji, amelisaidia cement kwa ajili ya kujengwa upya.


Mbunge Mohamed Dewji, akizungumza na waumini wa Kanisa la Pentekosti la kijiji cha Ititi muda mfupi kabla hajakabidhi msaada wa mifuko 25 ya saruji na shilingi laki tano taslimu.


Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohamed Gullam Dewji, akimkabidhi Mchungaji Daud Elia, mifuko 25 ya saruji kwa ajili ya kujengea Kanisa hilo.


Pikipiki 10, aina ya Sanlag CC150, zilizotolewa msaada ya Mbunge wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji kwa vikundi 10 vya wafanyabiashara wa bodaboda mjini Singida leo.


Mbunge wa Singida mjini, Mohammed Dewji, akicheza KIDUKU na baadhi ya wafanyabiashara wa bodaboda wa mjini Singida, kabla ya mbunge huyo, kuwakabidhi msaada wa pikipiki. 


Baadhi ya wafanyabiashara wa bodaboda, wakimsikiliza Mbunge wao, Mohamed Dewji, wakati alipokuwa akizungumza nao kabla ya kuwakabidhi pikipiki 10.


Mmoja wa wafanyabiashara wa bodaboda, akisoma risala yao kwa Mbunge wa Jimbo la Singida mjini Mohammed Gullam Dewji (mwenye kofia ya pama).

Mbunge wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji, akizungumza na wafanyabiashara wa bodaboda (hawapo kwenye picha), muda mfupi kabla kuwakabidhi msaada wa pikipiki 10, zenye thamani ya sh. milioni 20. Kushoto ni Katibu wa Umoja wa wafanyabiashara wa bodaboda, Maulid Mpondo na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Williamu Haaly na Katibu wa CCM wa Wilaya Singida.


Mbunge wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji, akimkabidhi Katibu wa Umoja wa Wafanyabishara wa Bodaboda, msaada wa pikipiki 10. (Picha zote na Geofrey Mwakibete na Nathaniel Limu)

No comments:

Post a Comment