Baadhi ya wagojwa waliopona FISTULA, wakiimba na kutoa ushuhuda wakati wa hafla hiyo, viwanjani hapo leo Juni 15,2012, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe ya Uzinduzi wa FISTULA, wakiwa pamoja na watoto wao wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika viwanjani hapo leo.
Daktari Bingwa wa upasuajji FISTULA katika Hospitali ya CCBRT, Dk. Robert Marenga (wa pili kulia), akitoa maelezo kwa Mama Salma na Mwenyekiti wa bodi ya hospitali hiyo, Dk. Wilbroad Slaam (kulia), wakati wa uzinduzi huo.
Mama Kikwete na Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT, Dk. Wilbroud Slaa (kulia), wakipata maelezo kutoka kwa Muelimishaji wa kitengo cha upasuaji Fistulahospitalini hapo.
Muelimishaji kutoka CCBRT (kushot), Seraphina Faya, akiwapa maelezo Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa bodi ya CCBRT, Dk. Slaa, wakati wa uzinduzi huo.
Mama Salma Kikwete, akimfurahia mtoto mchanga aliyembeba wakati wa uzindizi wa kamapeni ya matibabu ya Festula. Kusho ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Wilbroad Slaa.
Mama Salma Kikwete, akizunguma wakati akizindua kampeni ya matibabu ya Fistula jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT, Dk. Slaa.
Shuhuda wa mgojnwa wa Fistula, Beatrice Mlunga (kulia) pamoja na mume wake, Hosea Sanga na mtoto wao mchanga akitoa ushuhuda wakati wa uzinduzi wa kamepni hiyo leo, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akibonyeza kitufe ili kwa ajili ya kuliza king'ora cha uzinduzi wa kampeni hiyo ya Fistula. Kulia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sophia Mjema na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT, Dk. Slaa.
Msanii wa Mjomba band, Mrisho Mpoto, akitumbuiza katika hafla hiyo, viwanjani hapo leo.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akiimba pamoja na wasanii wa Kikundi cha Mjomba band, chini ya kiongozi wake, Mrisho Mpoto pamoja na wafanyakazi wa CCBRT wakati wa uzinduzi huo.
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Mojmba Band, wakitoa igizo la unyanyapaa wa ungonjwa wa Fistula, unaofanywa na baadhi ya watu, wakati wa uzinduzi huo viwanjani hapo leo.
No comments:
Post a Comment