Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda (katikati), akiwasha Mwenge wa Uhuru, kuashiria kuanza kwa mbio za mwenge huo, kwa mwaka 2012, leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mwenge huo utakimbizwa kwenye jumla ya Halmashauri za Wilaya, Manispaa na miji 157 na kuongozwa na kauli mbiu ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu Shiriki kuhesabiwa Agosti 26.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vipeperushi vya elimu ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchini kuanzia Agosti 26 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa mbio za mwenge leo jijini Mbeya.Kushoto anayeshuhudia uzinduzi huo ni Kamishna wa sensa kutoka ofisi ya taifa ya Takwimu, Hajjat Amina Fatma Mrisho.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara (Kushoto), akimtambulisha kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2012, Kepteni Honest Erenest Mwanossa (kulia), kutoka Dar es Salaam.
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka, Kepteni Honest Erenest Mwanossa kutoka Dar es Salaam akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, tayari kwa kuukabidhi kwa viongozi wa Mkoa wa Mbeya tayari kwa kuukimbiza kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2012, Kepteni Honest Erenest Mwanossa (kulia), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro, tayari kwa kuukimbiza kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, kabla ya kuelekea Mkoani Iringa.
Wananchi na Viongozi mbalimbali wakishuhudia shughuli za kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru leo jijini Mbeya.
Vijana wa kundi la halaiki kutoka katika shule mbalimbali za Mkoa wa Mbeya, wakipamba shughuli za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2012, zinazoongozwa na kauli mbiu ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu, Shiriki kuhesabiwa Agosti 26, leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya .
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, wakiwa wamevaa T-shirt zenye kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi 2012, leo jijini Mbeya, wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2012. Kutoka kushoto ni Luteni Mussa Ngomambo kutoka mjini magharibi Zanzibar, Sofia Kizigo kutoka Dar es salaam, Wito Mlemelwa kutoka Mbeya, akifuatiwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Kepteni Honest Mwanossa, Kajia Godfrey kutoka Shinyanga na Tatu Saidi Mussa kutoka Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar. (Picha zote na Aron Msigwa -MAELEZO)
No comments:
Post a Comment