Waendesha baiskeli inayoendeshwa na watu wawili, Jeremy Yamin (mbele) na Alicia Yamin, wakiwa tayari kwa matembezi hayo, Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini.
Mgeni rasmi katika matembezi ya baiskeli, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akisalimiana na Balozi wa Wapanda baiskeli duniani, Filberto Sebregondi (kushoto), wakati wa kuanza kwa matembezi hayo, yaliyokuwa yakihamasisha wananchi kupanda chombo hicho kwa ajili ya kuimarisha afya zao kimazoezi.
Mgeni rasmi katika matembezi ya baiskeli, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (wa pili kulia), akiwa Balozi wa Wapanda baiskeli duniani, Filberto Sebregondi (wa pili kushoto) pamoja na wapanda baiskeli wengine, wakiendesha baiskeli zao hizo kuelekea viwanja vya Biafra Kinondoni na kisha kurudi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini.
Balozi wa Wapanda baiskeli duniani, Filberto Sebregondi, akiwa amepanda baiskeli ya mmoja wa washiriki wa matembezi hayo, baada ya kumvutia kutokana na mapambo yake.
Msafari wa wapanda baiskeli, ukiongozw ana kijana aliyeuwa na ulemavu wa mguu mmoja, ukiwa njiani kuelekea Viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Msafara wa baadhi ya wapanda baiskeli, ukiwa na kijana wa miaka 5 (kulia), ukielekea kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupanda chombo hicho kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kuimarisha afya zao.
Baadhi ya wananchi wenye ulemavu wakiendesha baiskeli zao kwa ajili ya kushiriki matembezi hayo ya kuhamasisha upandaji baiskeli kama vyombo vingine vya usafiri.
Mgeni rasmi katika matembezi ya baiskeli, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akizungumza jambo na Balozi wa Wapanda baiskeli duniani, Filberto Sebregondi (kushoto), wakati wa matembezi hayo, maeneo ya Viwanja vya Biafra, Kinondoni.
Mgeni rasmi katika matembezi ya baiskeli, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akizungumza jambo na Profesa Karim, wakati matembezi hayo ya baskeli yalipofika kwenye viwanja vya Biafra, Kinondoni.
Balozi wa Wapanda baiskeli duniani, Filberto Sebregondi, akizunguma na wapanda baiskeli, wakati walipomaliza matembezi hayo Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi katika matembezi ya baiskeli, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akizungumza na wapanda baiskeli wakati wa kumalizika matebezi hayo, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika matembezi ya baiskeli, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akimkabidhi zawadi ya baiskeli, Desiberi Massawe baada ya kushinda katika bahati nasibu iliyochezeshwa viwanjani hapo, baada ya kumalizika matembezi hayo.
leo hakuna ok twasubiri kesho
ReplyDelete(mchumi shirikisho la vyuo DSM)