TANGAZO


Monday, May 28, 2012

SonGas yatoa taa 250 Mabwepande

Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Gaudentia Kabaka, akimkabidhi cheti cha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songas, Christopher Ford, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 


Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Songas Limited, leo imekabidhi taa 250 zinazotumia umeme wa sola kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaoishi kwenye kijiji cha Mabwepande kata ya Bunju B Manispaa ya Kinondoni. Wanafunzi hawa ni wale wanaotoka kwenye familia za wahanga wa mafuriko wanaoishi katika kijiji hicho cha Magwepande.

Hii ikiwa moja ya sehemu ya huduma kwa jamii inayofanywa na kampuni ya Songas Taa hizo zimekabidhiwa leo na Mratibu wa Mahusiano Jamii wa Songas Bw. Nicodemus Chipakapaka kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Songas Bw. Christopher Ford.

Aidha, Bw. Chipakapaka, aliongeza kuwa: “Taa zote 250 zina thamani ya Shilingi Milioni Ishirini (TSh20,000,000). Lengo la msaada huo nikuwasaidia wanafunzi wa sekondari na wanafunzi wa shule ya msingi hususani kwa wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya darasa la saba(7) na darasa la nne(4) ili waweze kujisomea nyakati za usiku na hivyo kufanya vizuri darasani na katika mitihani yao.”

Mkurugenzi huyo wa Songas Bw. Chiapakapaka aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam; Wilaya ya Kinondoni, serikali za mitaa, na uongozi wa shule zote mbili za Msingi na Sekondari kwa kuonyesha ushirikiano katika hatua zote za kukabidhi msaada huu.

“Nawashukuru sana kwa kufika na kushiriki katika zoezi hili muhimu la kusaidia jamii hii iliyopatwa na maafa mazito ya mafuriko. Kama kampuni Songas imeguswa sana na swala hili na inaungana na jamii yote ya Tanzania kuwapa pole,” alisema.

Kutokana na majukumu mbalimbali ya kijamii, Chipakapaka alisema kuwa Songas haitaweza kutoa taa hizi kwa kila familia hivo tunaomba kwa sasa tutoe taa hizi kwa familia zenye watoto wanao soma sekondari na shule ya msingi kuazia darasa la nne mpaka la saba.

“Mbali na kusaidi wanafunzi taa hizi zitasaidia sana wazazi ku-chaji simu zao na kuondoa uzia wanaopata kwasasa kwa kwenda kuchaji simu mbali na nyumbani,” alisema.

Bw. Chipakapaka pia aliwaasa wanafunzi kukazana na masomo kwani dunia ya leo na
ijayo inahitaji wasomi zaidi na elimu pekee ndio itawawezesha kufikia mafanikio na kuweza kusaidia wazazi na hata familia zao.

“Wanafunzi naomba mfanye bidii sana katika masomo kwani hii ndio silaha ya kujikomboa na umasikini kwenu wenyewe pamoja na familia zenu. Ni imani yangu taa hizi mtazitunza na kuzitumia vizuri, ” alisema.

No comments:

Post a Comment