
Wachezaji wa Yanga wakipiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya mchezo huo, kabla ya mpambano huo kuanza, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Wachezaji wa Simba wakipiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya mchezo huo, kabla ya mpambano huo kuanza, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Waamuzi wa mchezo huo wakipiga picha pamoja na manahodha wa timu hizo, Juma Kaseja wa Simba (wa pili kushoto) na Shadrack Nsajigwa (wa pili kulia), kwa ajili ya kumbukumbu ya mchezo huo.
Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom likiwa limewekwa Uwanjani kwa ajili ya kusubiri kukabidhiwa bingwa wa Ligi hiyo, baada ya mchezo kati ya timu hizo pinzani.
Mchezaji wa Simba, Patrick Mafisango, akipiga mpira huku akifuatwa na Nadir Haroub 'Canavaro' wa Yanga katika mchezo huo wa watani wa jadi, ambapo Yanga ilikubali kichapo cha mabao 5-0.
Nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa akijaribu kumtoka mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi katika mchezo huo.
Wachezaji wa Simba, Amir Maftah, Kazi Moto, Felix Sunzu (10) na Emmanuel Okwi (katikati aliyefichika wakishangilia goli la kwanza la timu hiyo lililofungwa na Okwi.
Shadrack Nsajigwa wa Yanga, akiudhibiti mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.
FelixSunzu wa Simba, akimtoka Oscar Nkulula wa Yanga katika mchezo huo.
Emmanuel Okwi wa Simba akishangilia goli lake la pili aliloifungia timu yake katika mpambano huo.
Mashabiki wa Simba wakishangilia goli la pili la timu hiyo dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mwamuzi wa mchezo huo, Hashim Abdallah, akimpa kadi ya njano golikipa wa timu ya Yanga, Said Kasalama baada ya kumdondosha Emmanuel Okwi alipokuwa ndani ya eneo la penalti na kisha kupigiwa adhabu hiyo, iliyopigwa na Patrick Mafisango na kufanya Simba hadi wakati huo kuongoza kwa mabao 3-0.
Kijana akiwa na mfano wa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, akilinyanyua juu huku akiwa amebebwa na baba yake, kwenye jukwa la mashabiki wa timu ya Simba, uwanjani hapo leo jioni.
Wachezaji wa Simba, wakiongozwa na nahodha wao, Juma Kaseja (katikati), wakishangilia goli la nne, alilolifunga kwa mkwaju wa penalti, baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa tena na beki Shadrack Nsajigwa.
Mashabiki wa Simba wakishangilia wakiwa na mfano wa kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Mashabiki wa Yanga wakiwa wameshikwa na butwaa baada ya kufungwa goli la tano na Felix Sunzu.
Mpaka dakika inayoonekana kwenye ubao wa matokeo, mabao yalikuwa kama inavyosomeka kwenye ubao huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenella Mukangala, akimkabidhi Nohodha wa timu ya Simba, Juma Kaseja Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, baada ya kuwatandika watani wao wa Jadi Yanga kwa mabao 5-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na hivyo kujikusanyia pointi 62 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine kwenye michuano hiyo, iliyomalizika leo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia na kombe lao la Ubingwa, mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala.
Baadhi ya mashabiki wa Simba wakipiga picha na kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu, lililonyakuliwa na timu hiyo, baada ya kuifunga Yanga mabao 5-0 katika mchezo wa kufunga ligi hiyo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wa pili kulia, aliyeshikilia kombe hilo ni Meneja wa Udhamini na Matukio wa Kampuni ya Vodacom, amabo ni wadhamini wa ligi hiyo, Ibrahim Kaude.
Wachezaji wa Simba wakipiga picha na kombe lao la Ubingwa mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo jioni.






















No comments:
Post a Comment