Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea taarifa ya utekelezaji wa kazi za Mkoa wa Kaskazini Unguja, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo, Pembe Juma Pembe, leo katika ukumbi wa Chuo cha Amali, Mkokotoni akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya miradi mbali mbali ya kijamii mkoani humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akizungumza na viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kaskazini B, ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni, akiwa katika ziara. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Mwinyihaji Makame, kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheir na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Pembe Juma Pembe.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna, akizungumza na wananchi wakati alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ili awasalimie Wananchi wa Matemwe Kigomani na kutoa nasaha zake wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la madarasa mapya katika Shehia hiyo,calipokuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya miradi mbalimbali ya kijamii Wilaya ya Kaskazini A.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wananchi wa Matemwe Kigomani katika ziara yake hiyo, mkoani humo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi wa Bwekunduni, baada kuizindua barabara ya kifusi katika shehia hiyo leo, alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, kuangalia maendeleo ya miradi mbalimbali ya kijamii katika wilaya ya Kaskazini A.

No comments:
Post a Comment