TANGAZO


Saturday, May 5, 2012

Rais Shein akutana na ujumbe wa Chuo Kikuu cha Saudia, mjini Zanzibar

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Dk. Fahad Hassan Arab, Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Elimu, wakati Ujumbe wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Saud Arabia, ulipofika Ikulu mjini Zanzibar, kuonana na Rais leo. Wa pili kulia ni Rais mstaafu wa Zanzibar na Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Abdullah Mohammed Mu'minah. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Saudi Arabia, ukiongozwa na    Rais mstaafu wa Zanzibar na Tanzania, Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia) na watatu ni Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Abdullah Mohammed Mu'minah na Naibu Katibu Mkuu wa huduma za Elimu wa Chuo hicho, Dk. Fahad Hassan Arab.

No comments:

Post a Comment