Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akishiriki kuimba wimbo wa wafanyakazi akiwa ameshikana mikono na Rais wa Jumuiya ya Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Omar Juma, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudence Kabaka (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa katika sherehe za Mei Mosi, Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Mei 1, 2012.
Baadhi ya Viongozi wa Mashirika, Makampuni na Idara mbalimbali sehemu za kazi, wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, jijini Tanga leo.
Baadhi ya wafayakazi wa sekta mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea kwenye maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi duniani 'Mei Dei', Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 3, kama zawadi kwa Mfanyakazi bora wa Tanesco, Anetha Chengula katika sherehe za Mei Mosi, Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akihutubia katika sherehe za Mei Mosi, Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Sekta na mbalimbali nchini wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete, wakati alipokuwa akiwahutubia katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani jijini Tanga leo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa wamekaa ubavuni mwa gari kubwa la Kampuni ya Simba Cemet, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga, wakimsikiliza mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Kitaifa, Rais Jakaya Kikwete, wakati alipokuwa akiwahutubia kwenye maadhimisho hayo leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwahutubia Wafanyakazi katika sherehe za maadhimisho ya Siku yao, Duniani Mei Dei, Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo. Kulia ni baadhi ya Wabunge wa Vyama mbalimbali vya Siasa waliokuwa wamehudhuria katika maadhimisho hayo.










No comments:
Post a Comment