TANGAZO


Tuesday, May 1, 2012

Makamu wa Rais, Dk. Bilal, azindua Chuo cha VETA, Manyara

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Balozi wa Korea Kusini, Young Hoon Kim, wakikata utepe kuzindua rasmi Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kilichojengwa Wilaya ya Babati, mkoani Manyara, wakati wa hafla ya ufunguzi jana, Aprili 30, 2012. (Picha na  Muhidin Sufiani-OMR)

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu na viongozi wa Chuo cha Veta na Serikali, baada ya ufunguzi rasmi wa Chuo hicho, uliofanyika jana Aprili 30, 2012 mkoani Manyara.

 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo kipya cha VETA, baada ya kukifungua rasmi Chuo hicho jana.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Ufundi wa magari wa Chuo kipya cha VETA, mkoani Manyara, kuhusu trekta dogo linalotumika kulimia na kupandia mbegu za mazao, wakati alipokuwa akitembelea na kukagua majengo mapya ya Karakana ya chuo hicho baada ya kukifungua rasmi jana Aprili 30, 2012.

No comments:

Post a Comment