TANGAZO


Tuesday, May 1, 2012

Rais Dk. Shein apokea maandamano ya Wafanyakazi Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungia mkono, wafanyakazi wakati alipokuwa akipokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mayday), yaliyofanyika katika Viwanja vya Ukumbi wa Bwawani Hotel, mjini Zanzibar leo. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungia mkono, wafanyakazi wakati alipokuwa akipokea maandamano yao ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani 'Mei Dei'  mjini Zanzibar leo.

Wafanyakazi wa  Wizara ya Katiba na Sheria, wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), akiwa mgeni rasmi katika  Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani, Viwanja vya Ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel, mjini Unguja, zilizofanyika zilizoadhimishwa duniani kote leo.

 Wafanyakazi wa  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika  Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani katika Viwanja vya Ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel, mjini Unguja leo.

Wafanyakazi wa  Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kuadhimisha siku hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati ) akishikana mikono na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani na kuimba wimbo wa Mshikamano (Solidariti Foreva), unaotumiwa na wafanyakazi wote duniani huku wakinyanyua juu mikono yao, kuonesha mshikamano kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel, mjini Unguja zilikofanyika sherehe hizo leo.

 Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao katika maadhimisho ya
Siku ya Wanyakazi Duniani, mjini Zanzibar.

 Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao katika maadhimisho hayo.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi, Fedha tasilim, sh. 250,000,  Mfanyakazi Bor wa Halmashauri  ya Wilaya ya Magharibi kupitia Chama cha wafanyakazi cha ZALGWU, Kidawa Juma Said,  akiwa ni miongoni mwa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012, wakati wa Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Hotel Bwawani, mjini Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Fedha tasilim, sh. 500,000, Khamis Haji Mikidadi wa Ofisi ya Rais Ikulu, baada ya kuibuka mfanyakazi bora kwa mwaka 2012, kupitia Chama cha wafanykazi cha ZUPHE,   wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel, mjini Unguja.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Fedha tasilim, sh.700,000, Margreth Peter Mathew wa Nelia Hotel & Resort Zanzibar, akiwa ni mfanyakazi bora kupitia Chama cha Wafanykazi cha CHODAU, wakati wa sherehe hizo, mjini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wanayakazi wa Sekta mbalimbali za Serikali na Binafsi, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani 'MEI DEI', zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel, mjini Unguja. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar, Zahrani Mohamed Nassor, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman.

No comments:

Post a Comment