Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Paul Chizi akiongea na waandishi wa habari mara bada ya kuwasili kwa ndege mpya aina ya Boeing 737-500, Dar es Salaam leo, iliyokodishwa na shirika hilo, yenye uwezo wa kubeba abiria 108. (Picha na Mpiga picha wetu)
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), wakishuka katika ndege mpya aina ya Boeing 737-500, iliyokodishwa na shirika hilo yenye uwezo wa kubeba abiria 108. Ndege hiyo itaanza kuruka bada ya wiki moja.
Mmoja
wa wafanyakazi wa ATCL, akiwa amebeba ujumbe wa kumkaribisha Waziri
Harisson Mwakyembe baada ya uteuzi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete
hivi karibuni.
Wahudumu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), wakipozi mbele ya kamera, baada ya nde iliyokodishwa na shirika hilo, kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere, Dar es Salaam leo .
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), wakikata keki kusherekea ujio wa ndege ndege mpya aina ya Boeing 737-500. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Paul Chizi.
No comments:
Post a Comment