Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Rukwa (RPC), Sunto Mantage, wakiimba wimbo wa Utii wa Jeshi la Polisi kabla ya Mkuu huyo wa Mkoa kuzungumza na Polisi jana kwa ajili ya kujadili azma yake ya kuboresha makazi ya Polisi. Alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa nyumba za jeshi hilo na hata hizo zilizopo sio muafaka sana. Katika mpango huo maoni mbalimbali yalitolewa ikiwemo Polisi wenyewe kujitolea nguvu kazi kwa kufyatua matofali na michango fedha kabla ya kuwashirikisha wadau wengine katika kuchangia zoezi hilo. Katika kuhakikisha zoezi hilo linaaanza mara moja Injinia Manyanya alitoa ahadi ya kuchangia shilingi milioni 3.5. (Picha na mdau wetu)
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya, akizungumza na Askari Polisi wa Mkoa huo jana, ambapo alitangaza rasmi mpango wa Rukwa Salama. Katika mazungumzo hayo aliwataka askari wote kuwa na moyo wa kizalendo kwa kuipenda nchi yao na Serikali kwa ujumla. Pia aliwataka Polisi wahamasishe familia zao kwa ajili ya kushiriki katika zoezi lijalo la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika nchini kote tarehe 26 Agosti 2012.
Sajenti Bahati, akionesha vifaa alivyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa kwa wapiganaji wenzake. Alimshukuru Mkuu huyo na kusema kuwa yeye ni Kiongozi wa mfano kwani hawajawahi kuona Mkuu wa Mkoa akizungumza na Jeshi la Polisi hapo awali katika Mkoa huo.
Baadhi ya Askari Polisi, walioshiriki katika kikao hicho, wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa.





No comments:
Post a Comment