Patrick Mafisango enzi za uhai wake, akiichezea timu yake ya Simba. Leo hatunaye tena baada ya kupata ajali ya gari iliyochukua uhai wake, gari alilokuwa akiliendesha mwenyewe akitokea Maisha Club, Masaki jijini Dar es Salaam. Maisha mchezaji huyu atakumbukwa na Watanzania hususan wanachama na mashabiki wa timu ya Simba, aliyokuwa akiichezea kwa juhudi na bidii zote ili kuipatia mafanikio mpaka kifo kilipomchukua. Mungu ailaze mahali pema roho yake. Amina. (Na Mkurugenzi wa www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi wa mtandao wa Fullshangweblog, John Bukuku kulia akizungumza na Katibu Mkuu wa timu ya Simba, Evodius Mtawala, wakati Katibu Mkuu huyo, alipokuwa akielezea mipango ya kuuhifadhi na kuusafirisha mwili wa mchezaji wao, marehemu Patrck Mafisango Mutesa, aliyeafiki alfajiri ya usiku wa kuamkia leo maeneo ya Chang'ombe Veta jijini Dar es Salaam, wakati akirejea nyumbani kwake, akitokea ukumbi wa burudani wa Maisha Club, Masaki na kusababisha watu wengine aliokuwa nao kupata majeraha. Mtawala amesema hayo, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam na kueleza kwamba kwa sasa wanawasiliana na Ubalozi wa Rwanda na mashirika ya ndege ili kukamilisha utaratibu wa vibali mbalimbali tayari kwa kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda nchini Rwanda kwa mazishi na taarifa kamili ya lini utasafirishwa, alisema itatolewa kesho mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote, katika picha kushoto ni mmoja wa mashabiki wa Simba aliyefika Muhimbili kushuhudia kilichotokea.
Mchezaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi 'Boban' akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na jamaa na marafiki baada ya kushuhudia mwili wa mchezaji mwenzake, marehemu Patrick Mafisango katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .
Wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga (kushoto) na Uhuru Selemani wa Simba wakisikitika wasijue la kufanya baada ya kushuhudia mwili wa mchezaji mwenzao marehemu Patrick Mafisango katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili leo.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Ngonyani 'Profesa Maji Marefu', akizungumza na wanaandishi wa habari hospitalini hapo, kuelezea masikitiko yake juu ya kifo cha mchezaji huyo.
Mchezaji wa Simba, Haruna Moshi akitoka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti huku akilia kwa uchungu baada ya kuhakikisha Patrick Mafisango amefariki.
Mchezaji wa Simba, Haruna Moshi akihojiwa, alijaribu kuongea lakini akashindwa.
Mchezaji Uhuru Selemani wa Simba, akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na mmoja wa waombolezaji.
Mchezaji wa zamani wa Simba Boniface Pawasa, akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga. Pawasa amesema jana usiku walikuwa naye kwenye muziki katika klabu ya Maisha Oysterbay wakati bendi ya Akudo Impact ikifanya onesho klabuni hapo na marehemu alimuaga kwamba anaenda nyumbani baadae akapigiwa simu kwa simu ya marehemu akiambiwa mwenye simu hiyo, amefariki dunia kwa ajali.
Boniface Pawasa kushoto na Uhuru Selemani wakilia.
Mchezaji Uhuru Selemani, akisalimiana na wanamuziki wa bendi ya Akudo Impact ambao pia wameelezea masikitiko yao kwani wamesema marehemu walikuwa naye usiku wa kuamkia leo katika klabu ya Maisha ambako walikuwa wakifanya onyesho lao.
Aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Simba Mrundi Ramadhana Wasso, akihojiwa na waandishi wa habari kuelezea masikitiko yake kutokana na msiba huo.
Mashabiki wa Simba wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo, wakiwa na masikitiko makubwa kwa kuondokewa na mchezaji wao kipenzi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo asubuhi.(Picha na Fullshangwe Blog)

No comments:
Post a Comment