TANGAZO


Thursday, May 17, 2012

Tanzania kuwa mwenyeji mikutano ya mwaka 2012 ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB)

  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB),Tonia Kandiero, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha, Dar es Salaam leo, wakati Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (kushoto), alipokuwa akitangaza kufanyika kwa mikutano ya benki hiyo, jijini Arusha kuanzia Mei 28 hadi Juni 1, 2012, ambapo mkutano huo Tanzania imekuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza tangu benki hiyo kuanza shughuli zake mwaka 1971 hapa nchini. Mikutano hiyo itakayofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimatifa (AICC), Arusha na kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete Mei 31. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Ofisa Mipango wa Nchi wa benki hiyo, Projesh Bhakta (kushoto), akiwa na baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Fedha, wakati wa mkutano huo, wizarani hapo leo.

 Mwandishi wa Radio Uhuru (Uhuru FM), Cecilia Jeremiah, akiuliza swali kuhusu urari wa fedha iliyonao benki Kuu huku Tanzania ikiwa ni mwenyeji wa mikutano benki hiyo.

 Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huo, wakati akitoa taarifa hiyo leo asubuhi. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB),Tonia Kandiero.

 Ofisa Mipango wa Nchi wa benki hiyo, Projesh Bhakta (kushoto), akifuatilia mazungumzo hayo pamoja na baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Fedha, wakati wa mkutano huo, wizarani hapo leo.

 Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano huo waliotaka kujua habari mbalimbali kuhusiana na mikutano hiyo ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), itakayofanyika jijini Arusha Mei 28 hadi Juni 1. Kulia kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Silvanus Likwilile na Ofisa wa Wizara, Jerome Bureta.

 Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, kwenye mkutano huo, aliokuwa akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa mikutano ya Bodi ya Magavana ya AfDB na Mfuko wa Maendeleo Afrika jijini Arusha.

Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, akibadilishana mawazo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Tonia Kandiero, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao na waandishi wa habari, wizarani hapo leo.

No comments:

Post a Comment