TANGAZO


Thursday, May 31, 2012

Dk. Shein azungumza na Wahariri, Waandishi wa habari


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed
Shein, akizungumza  na Wahariri na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Bara na Visiwani katika ukumbi wa Ikulu mjini Zanzibar leo kuhusu uvunjiu wa amani na vitendo vya ukiukwaji wa sheria vilivyofanywa na baadhi ya wananchi kisiwani Unguja juzi. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)


Baadhi ya Wahariri na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya Serikali na Binafsi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed
Shein, alipokuwa akizungumza nao leo, ukumbi wa Ikulu, mjini Zanzibar.  

Mwandishi wa Kampuni ya IPP Media, Farouk Karim, akiuliza swali wakati Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao kuhusu vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyofanywa na baadhi ya wananchi, visiwani humo juzi. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifafanua jambo kwa wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali, wakati alipokuwa akizungumza nao, Ikulu  mjini Zanzibar leo.

No comments:

Post a Comment