TANGAZO


Wednesday, May 16, 2012

CHANETA chawashukuru wadau wa Netiboli

 Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akiwashukuru wananchi mbalimbali waliowaunga mkono na kujitolea kwa hali na mali katika kufanikisha mashindano ya mpira huo kwa nchi za Afrika, yaliyofanyika nchini na kumalizika hivi karibuni, ambapo timu ya Malawi iliibuka bingwa na Tanzania kushika nafasi ya pili. Katikati ni Katibu Mkuu wa Chaneta, Rose Mkisi na kulia ni mjumbe wa Chama hicho, Mwajuma Kisengo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Mshauri wa Chama cha Mpira wa Netiboli Tanzania (CHANETA), Joel Mwakitalu, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano wa kuwashukuru wananchi mbalimbali waliowaunga mkono na kujitolea kwa hali na mali katika kufanikisha mashindano ya mpira huo kwa nchi za Afrika, yaliyofanyika nchini na kumalizika hivi karibuni, ambapo timu ya Malawi iliibuka bingwa na Tanzania kushika nafasi ya pili. Katikati ni Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi na Katibu Mkuu wake, Rose Mkisi.

Katibu Mkuu wa CHANETA, Rose Mkisi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati uongozi wa chama hicho ulipokuwa ukiwashukuru wananchi mbalimbali waliowaunga mkono na kujitolea kwa hali na mali katika kufanikisha mashindano ya mpira huo kwa nchi za Afrika, yaliyofanyika nchini na kumalizika hivi karibuni, ambapo timu ya Malawi iliibuka bingwa na Tanzania kushika nafasi ya pili. Katikati ni Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi, na kushoto ni Mshauri wa CHANETA, Joel Mwakitalu.
  
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati alipozungumza nao, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akiwashukuru wananchi mbalimbali waliowaunga mkono na kujitolea kwa hali na mali katika kufanikisha mashindano ya mpira huo kwa nchi za Afrika, yaliyofanyika nchini na kumalizika hivi karibuni, ambapo timu ya Malawi iliibuka bingwa na Tanzania kushika nafasi ya pili. Kulia ni Katibu wake Mkuu, Rose Mkisi.

Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi, akijibu maswali ya waandishi wa habari, kwenye mkutano huo. Katikati ni Mshauri wa CHANETA, Joel Mwakitalu na .kushoto ni mjumbe wa Chama hicho, Rose Kisiwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi, akiomba mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, ili kushukuru kwa kufanikiwa kuyaendesha mashindano ya Ubingwa wa mchezo huo, barani Afrika kwa ufanisi.Katikati ni Katibu Mkuu wa Chaneta, Rose Mkisi na kulia ni mjumbe wa Chama hicho, Mwajuma Kisengo.
Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi pamoja na Katibu wake Mkuu, Rose Mkisi (katikati) na mjumbe wa Chama hicho, Mwajuma Kisengo, wakisali kwa ajili ya kumshukuru Mungu, wakati wa mkutano huo wa kuwashukuru wadau wa mchezo huo kwa kuchangia kwa hali na mali katika kufanikisha mashindano hayo. 

Baadhi ya waandishi wa habari, wliokuwepo kwenye mkutano huo, nao wakisali kwa ajili ya kumshukuru Mungu.

Mwenyekiti wa CHANETA), Anna Bayi, akinyanyua juu chupa yake ya soda kwa ajili ya kuonesha furaha yake pamoja na waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho kwa kufanikisha mashindano ya Ubingwa huo.

No comments:

Post a Comment