TANGAZO


Wednesday, May 9, 2012

Basi la Muro lateketea kwa moto, Morogoro


Basi la kampuni ya Kampuni ya  Muro Investment, T 820 BEY lillilokuwa likitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Abiria wote walinusurika katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku Mei 8, 2012, isipokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto huo. 

Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto. (Picha zote na mdau wetu)

Hali ya moto ilivyokuwa ikibadilika kila muda ulivyokuwa ukienda.
Hapa likiwa limeteketea kabisa, vikiwemo mizigo yote na vifaa vingine vya abiri waliokuwemo kwenye basi hili.

No comments:

Post a Comment