Baadhi ya Masheikh waliohudhuria katika Mkutano wa Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakari Khamis Bakari, wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliokuwa yakitolewa kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar. (Picha na Mpigapicha Wetu)
Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari, akifafanua jambo katika mkutano na Masheikh wa Jumuiya mbalimbali za Kiislam, kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud na kushoto ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud, akifafanua jambo katika mkutano na Masheikh wa Jumuiya mbalimbali za Kiislam, kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar. Kushoto ni Waziri Katiba na Sheria wa Zanzibar Abubakar Khamis na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame.
Amiri kutoka katika Jumuiya ya Uamsho, Mselem Ali, akielezea jambo katika mkutano na Waziri wa Katiba na Sheria Abubakari Khamis, kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu CUF, Ismail Jusa Ladhu, akifafanua jambo katika mkutano na Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakari Khamis Bakari, kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
No comments:
Post a Comment