TANGAZO


Friday, April 27, 2012

Waziri Nchimbi ashuhudia kupatikana mshindi wa Jishindie Mchongo

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Corporation, wachapishaji wa Magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa na The African, Prince Bagenda (katikati), mara baada ya kuwasili katika Ofisi za kampuni hiyo, kushuhudia upatikanaji wa mshindi wa bahati nasibu ya 'Jishindie Mchongo', ambayo mshindi wake, anajinyakulia gari, lenye thamani ya sh. milioni 8, shindano lililowashirikisha wasomaji wa magazeti hayo na kufikia tamati leo, kwa kuchezesha bahati nasibu hiyo. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)




Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari, mara baada ya kutembelea chumba cha habari cha New Habari Corporation, wachapishaji wa Magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa na The African. Kutoka kulia ni Mhariri Mtendaji wa Magazeti hayo, Prince Bagenda  na Mkurugenzi Mtendaji, Hussein Bashe.




Mratibu wa shindano la 'Jishindie mchongo', lililowahusisha wasomaji wa Magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa na The African, Essu Ogunde, akichanganya karatasi zilizojazwa na wasomaji, tayari kwa kuchagua mshindi wa zawadi ya gari aina ya Vitz, lenye thamani ya sh. milioni 8 leo, jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari, Hussein Bashe.




Mkurugenzi Mtendaji  wa New Habari Corporation, Hussein Bashe (kushoto), akimpigia simu mshindi wa zawadi ya gari, aina ya Vitz, kwenye  shindano la 'Jishindie mchongo' , Kassim Ramadhani, mkazi wa eneo la Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuponi yake kuibuliwa na kushinda gari hilo. Anayeiangalia kuponi hiyo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) na Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo, Godbless Urassa.




Wafanyakazi wa New Habari Corporation, wakifuatilia kwa makini uchezeshwaji wa bahati nasibu hiyo leo, Ofisi za Kampuni hiyo, Sinza Kijiweni, jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa  Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam, Kassim Ramadhani, ameibuka mshindi wa gari.





Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, akiliangalia gari atakalokabidhiwa  mshindi  shindano la 'Jishindie Mchongo', lililoandaliwa na kampuni ya New Habari Corporation, wachapishaji wa Magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa, na The African leo, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment