Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Vijana Dk. Kissui Steven, akiongea na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu sherehe za kuwashwa Mwenge wa Uhuru, zitakazofanyika mkoani Mbeya, Mei 11, mwaka huu. Na kuelezwa kuwa moja ya kauli mbiu zake, itakuwa ni katika kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi, litakalofanyika nchini kote, kuanzia Agosti 26, mwaka huu. Kulia ni Afisa Uhamasishaji wa Sensa ya watu na makazi, Said Amir. (Picha zote na Anna Nkinda-Maelezo)
Mratibu wa Sensa ya watu na makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Irenius Ruyobya, akiongea na waandishi wa habari leo jijini, kuhusu umuhimu wa wananchi kujibu kwa ufasaha maswali watakayoulizwa, wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi, litakalofanyika nchini kote, kuanzia Agosti 26, mwaka huu. Jumla ya shilingi bilioni 141 imeelezwa kuwa zitatumika mpaka kukamilika kwa zoezi hilo.
Afisa Uhamasishaji Sensa ya watu na makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Said Amir akiwashukuru waandishi wa habari, kutokana na jitihada zao za kuwaelimisha wananchi kuhusiana na zoezi la sensa ya watu na makazi, litakalofanyika nchini kote, Agosti 26, mwaka huu. Hii ni Sensa ya tano kufanyika hapa nchini tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961.
Afisa Uhamasishaji Sensa ya watu na makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Said Amir, akiwaonesha waandishi wa habari, vitabu vyenye maelezo mbalimbali kuhusiana na sensa ya watu na makazi, itakayofanyika kote nchini kuanzia Agosti 26, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment