TANGAZO


Friday, April 27, 2012

Waziri Nagu afungua Kongamano la Makatibu Muhtasi Mwanza


Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Makatibu Muhtasi nchini, linalofanyika leo  Ukumbi wa Hoteli ya Malaika, jijini Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji,  Dk. Mary Nagu (katikati), akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Eng. Evarist Ndikilo pamoja na wadau wengine wa Kongamano hilo wakati akiwasili kwenye hoteli hiyo leo. (Picha na Mpigapicha Wetu)


Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA), Pili Penda (kulia), akimpokea Mgeni rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi nchini, linalofanyika leo kwenue Ukumbi wa Hoteli ya Malaika, jijini Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu.


Mshereheshaji Ephraim Kibonde, akizungumza wakati wa ufunguzi wa  kongamano hilo, kabla mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu hajalifungua, jijini Mwanza leo.


Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA), Pili Penda, akitoa maelezo mafupi kuhusu kongamano hilo kwa Mgeni rasmi, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, wakati wa ufunguzi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Beach Resort, jijini Mwanza.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu akiwahutubia wajumbe wa mkutano huo, wakati akilifungua kongamano hilo leo, Aprili 27, jijini humo.


 Baadhi ya wajumbe mbalimbali wa mkutano huo, wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, wakati alipokuwa akiliungua kongamano hilo.


 Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo, wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli hiyo, wakimsikiliza Waziri Dk. Mary Nagu, alipokuwa akiwahutubia kwenye kongamano hilo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, akiionesha tuzo ya heshima, aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA), Pili Penda (kulia), mara baada ya kulifungua kongamano la Makatibu hao.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo, mara baada ya kuufungua, Hoteli ya Malaika Beach Resort, jijini Mwanza, leo.

No comments:

Post a Comment