TANGAZO


Friday, April 27, 2012

Mkuu wa Mkoa Rukwa Eng. Manyanya, aonana na Mkuu wa Majeshi ya akiba Bg. Gen. Muhuza



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya, akizungumza na Mkuu wa Jeshi la akiba nchini, Brigedia Generali R. M Muhuza (hayupo pichani), katika Ofisi yake leo, alipomtembelea kujitambulisha na kueleza juu ya ujio wake Mkoani Rukwa,  ambapo alisema ni kuona matayarisho ya kikosi cha mgambo cha Mkoa wa Rukwa ambacho kitashiriki kwenye zoezi la kijeshi litakalohusisha vikosi vya JWTZ, vilivyopo katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ambayo ni pamoja na Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa, Lindi, Mtwara, Njombe na Katavi,  ifikapo Septemba 15, 2012. Zoezi hilo la kijeshi litaandaliwa na Brigedi ya 401 KV, iliyopo Songea, mkoani Ruvuma. Jumla ya Wanamgambo 60, kutoka Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo, litakalojumuisha vikundi toka Kamandi zingine za Ndege za Kivita, Wahandisi, Mizinga na Vifaru.


Kutoka kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Akiba nchini, Brigedia Generali R. M Muhuza, Msaidizi wake Kanali A.Y Amasi na Katibu wake Meja A. R Gumbo, kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Dar es Salaam wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa walipomtembelea ofisini kwake leo.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya, akizungumza na Ujumbe huo wa Jeshi, uliomtembelea ofisini kwake leo.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya, akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo, ikiwemo uboreshwaji wa sekta muhimu nchini, kama sekta ya ulinzi ili kuepusha uvunjifu wa amani iliyodumu nchini kwa muda mrefu. Alisema Jeshi la Wananchi lina jukumu kubwa la kuhakikisha amani na utullivu unakuwepo nchini na kufafanua kwamba sio tu hatari zinazoweza kutoka nje bali na kwa hatari zinazoweza kusababishwa na wananchi wenyewe. (Picha na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa RUKWA)

No comments:

Post a Comment