Hii ni moja ya picha kubwa iliyochorwa katika ukuta wa bweni ambalo wanalala watoto wa kituo cha Miyuji kilichopo katika eneo la Miyuji, mkoani Dodoma. Kituo kinachoendeshwa na Kusimamiwa na Kanisa Katoliki.
Mbuzi huyo alikua ni moja ya Zawadi ya Pasaka kutoka kwa wanafunzi wa UDOM waliyopelekewa watoto waishio katika mazingira magumu katika Kituo cha kulelea Watoto cha Miyuji kinachosimamiwa na Kanisa Katoliki kilichopo Miyuji Mkoani Dodoma.
Wanafunzi wa UDOM, wakiwa wamewasili katika Kituo cha watoto yatima cha Miyuji na kiroba cha Unga kama moja ya zawadi walizowapelekea watoto hao, wakati walipotembelea kituo hiko cha miyuji kilichopo, maeneo ya Miyuji mkoani Dodoma.
Watoto waishio Katika kituo Cha Kulelea watoto Cha Miyuji Wakiwa wamekusanyika mara baada ya Wanafunzi wa UDOM kuwasili katika Kituo hiko kilichopo maeneo ya Miyuji Mkoani Dodoma hapo Jana
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa pamoja na watoto waishio kituoni hapo katika moja ya Mashamba ya machungwa yaliyopo kituoni hapo wakti wanafunzi wa UDOM walipokwenda kuwatembelea Watoto hao hapo jana
Wanafunzi wa UDOM, wakicheza na yatima wa kituo cha Miyuji, mkoani Dodoma wakati walipowatembelea kituoni hapo, ambapo walitoa zawadi ya Pasaka kwa watoto hao. |
Picha juu ni wanafunzi wa UDOM wakishiriki kuimba pamoja na Watoto hao katika kituo hicho ambapo wanafunzi wa UDOM walienda kuwatembelea watoto hao jana na kucheza nao baadhi ya michezo.
Baadhi ya Wanafunzi wa UDOM, wakiwa katika picha ya pamoja na watoto waishio katika kituo cha Miyuji kilichopo maeneo ya Miyuji, mkoani Dodoma wakati wanafunzi wa UDOM walipokwenda kuwatembelea Watoto hao hapo jana. (Picha zote na Fadhil Gharib Linga Wa Lukaza Blog)
No comments:
Post a Comment