TANGAZO


Saturday, April 14, 2012

Wanafunzi wa Sosholojia, UDOM watembelea, watoa misaada Hospitali ya Milembe


Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakishuka kwenye basi, walipowasili Hospitali ya wagonjwa wa akili ya Milembe, mjini Dodoma leo, kwa ajili ya kuwatembelea, kuwajulia hali na kuwapa misaada mbalimbali. (Picha Zote na Josephat Lukaza)
Wanafunzi wa wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), walipowasili katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Milembe iliyopo Dodoma kwa ajili ya kuwatembelea na kukabidhi misaada yenye thamani ya jumla ya shiling laki tano na nusu.


 Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Milembe, Dk. John Ndimo, akiongea na wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), walipokwenda kutembelea hospitali hiyo kwa lengo la kutoa msaada na kujifunza. Wa pili kulia ni Msemaji wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Sosholojia chuoni,  Leo Joachim.


Msemaji wa Taasisi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMSSO), Leo Joachim akiongea na Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Milembe, iliyopo mkoani Dodoma, mbele ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya kwanza ya Sosholojia kutoka Chuo kikuu hicho (hawapo pichani)


Baadhi ya Wanafunzi wanaosomea Shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha Dodoma, wakimsikiliza kwa makini, Muuguzi Mfawidhi wa hospitali ya Milembe wakati alipokua akieleza hali halisi ya hospitali hiyo leo.


Katibu wa taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya kwanza ya Sosholojia, Chuo Kikuu cha Dodoma, Mirobo Mashauri, akijiandaa kukabidhi misaada iliyotolewa  na wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu hicho, wakati walipotembelea hospitali ya Milembe leo.


Katibu wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma,  Mirobo Mashauri (kushoto), akikabidhi baadhi ya misaada iliyotolewa na Wanafunzi hao, wakati walipotembelea hospitalini hipo leo.


 Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Milembe Dk. John Ndimo (wa tatu kulia) akishukuru kwa misaada iliyotolewa na wanafunzi hao, wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia, Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), wakati walipotembelea hospitali hiyo.


Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma, wakisikiliza kwa makini maelezo ya Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Milembe iliyopo mkoani  Dodoma, wakati wanafunzi hao, walipozuru hospitalini hapo.


Afisa Habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO), akiongea na ITV wakati wa ziara ya wanafunzi wa Sosholoji, hospitalini hapo. 


Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma, Gaudensia Mwakemwa akiongea na ITV wakati wa ziara ya Wanafunzi hao, hospitalini hapo. 


Baadhi ya wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), wakiwa hospitalini hapo leo.


 Gari lililowabeba wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), likirudi chuoni, mara baada ya kumalizika kwa shughuli mbalimbali, walizokuwa wakizifanya hospitalini hapo. 

No comments:

Post a Comment