Mfanyabiashara maarufu nchini, na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mustafa Sabodo (kushoto), akitia saini hundi yenye thamani ya sh. mil. 100, alizotoa msaada kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kufurahishwa na ushindi wa chama hicho katika uchaguzi wa Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Jumapili iliyopita. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Antony Komu. Hafla hiyo imefanyika leo nyumbani kwa Sabodo Upanga, Dar es Salaam. (Picha na Richard Mwaikenda)
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa (kulia),
akimshukuru mfanyabiashara maarufu nchini na Kada wa CCM, Mustafa Sabodo baada ya kukipatia chama hicho, msaada wa sh. mil. 100, kutokana na kufurahishwa na ushindi wake kwenye uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki Jumapili iliyopita.
No comments:
Post a Comment