Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Upendo Nkone, akimba pamoja na mashabiki wa muziki huo, katika Tamasha la muziki la Pasaka linalofanyika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma usiku huu. Jana tamasha hilo lilifanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waimbaji maarufu kutoka nje ya Tanzania na ndani. (Picha na John Bukuku)
Mwimbaji wamuziki wa Injili, Upendo Nkone akicheza kwa mfuraha na mashabiki wake wakati akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku huu.
Mashabiki wakiwa wameketi kwenye viti vyao katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, wakifuatilia tamasha hilo.
Mwimbaji Anastazia Mukabwa kutoka nchini, Kenya akishambulia jukwaa huku mashabiki wakijongelea kwenye jukwaa kwa ajili ya kumuona kwa karibu, wakati alipokuwa akiimba wimbo unaoitwa 'Vua viatu'.
Mwimbaji Anastazia Mukabwa kutoka nchini Kenya naye akiimba pamoja na mashabiki wake, wakati akitumbuiza kwenye tamsha hilo. |
Kundi la Worriars Band, likifanya vitu vyake jukwaani kama linavyoonekana katika picha hii.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akifafanua jambo kwa MC wa Tamasha hilo MC Mwakipesile. Katikati ni mratibu wa Tamasha hilo, Hudson Kamoga.
No comments:
Post a Comment