TANGAZO


Monday, April 9, 2012

Pinda atoa pole msiba wa Kanumba, awasili Dodoma tayari kwa vikao vya Bunge


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya waombolezaji wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba Sinza Vatican, jijini Dar es salaam leo Aprili 9, 2012, kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu huyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisaini kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa  mwigizaji  mahiri nchini, marehemu Steven  Kanumba, nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda  akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo, Aprili 9,2012 kuhudhuria kikao cha Bunge, kinachotarajiwa kuanza Aprili 10, 2012. 

No comments:

Post a Comment