TANGAZO


Tuesday, April 17, 2012

Songas yakabidhi madarasa, Ofisi na madawati, Shule ya msingi Kibamba

Kaimu Afisa Elimu,  wilayani Mkuranga, Teddy Bagolele, akikata utepe kuzindua madarasa mawili, yenye madawati hamsini kila moja pamoja na Ofisi ya walimu katika shule ya Msingi Kibamba, Mkuranga, mkoani Pwani, yaliyojengwa na Songas na kugharimu sh. milioni 20, wakati wa hafla ya makabidhiano shuleni hapo leo. Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Songas, Nicodemus Chipakapaka. (Picha na Mdau wetu)





Afisa Maendeleo ya Jamii wa Songas, Nicodemus Chipakapaka, akiwa katikati ya wanafunzi, baada ya kukabidhi madarasa mawili, madawati mia moja na chumba  cha Ofisi ya walimu katika shule ya Msingi ya Kibamba, wilayani Mkuranga leo. Majengo hayo pamoja na madawati yamegharimu jumla ya sh. millioni 20. 

No comments:

Post a Comment