Emmanuel Okwi wa Simba (kulia), akimtoka Issac Seun-Maliki wa Al Ahly Shandy katika mchezo huo.
Wachezaji wa Simba, wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo, dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan, lililofungwa na Haruna Moshi (3), aliyebebwa na wachezaji Felix Sunzu na Uhuru Suleiman (kulia), huku Emmanuel Okwi (kushoto), akijiunga nao kushangilia.
Issac Seun-Maliki wa Al Ahly Shandy, akijaribu kuondoa mpira miguuni mwa Felix Sunzu wa Simba.
Haruna Moshi 'Boban', wa Simba akimtoka Sadam Abutalib wa Al Ahly Shandy.
Haruna Moshi 'Boban', wa Simba akiwatoka, Sadam Abutalib (kushoto) na Zakaria Nasu wa Al Ahly Shandy.
Felix Sunzu wa Simba, akimtoka Faris Abdallah wa Al Ahly Shandy ya Sudan katika mchezo huo, uliokuwa wa vuta nikuvute.
Felix Sunzu, akijaribu kumuhadaa Issac Seun-Maliki wa Al Ahly Shandy.
Issac Seun-Maliki wa Al Ahly Shandy, akipambana na Haruna Moshi 'Boban', wa Simba.
Felix Sunzu, akikimbiza mpira na kapteni wa timu ya Al Ahly Shandy, El Nuru Altigani.
Baadhi ya Maofisa wa benchi la Ufundi la timu ya Al Ahly Shandy, wakiwa hawaamini macho yao baada ya timu yao kukubali goli la tatu, lililofungwa na Emmanuel Okwi.
Uhuru Suleiman wa Simba, akipambana na Issac Seun-Maliki wa Al Ahly Shandy.
Emmanuel Okwi (kushoto) na Patrick Mafisango wakishangilia bao la pili la timu hiyo, lililofungwa na Mafisango.
Uhuru Suleiman, Shomari Kapombe, Felix Sunzu na Patrick Mafisango, wakishangilia goli la tatu la timu hiyo.
Hadi mwsiho wa mchezo huo, ubao wa matokeo kwenye Uwanja wa Taifa, uliokuwa ukisomeka hivi.
Kapteni wa timu ya Simba, akiwapungia mashabiki baada ya mchezo huo, kumalizika na timu yake ya Simba kuibuka na karamu ya mabao 3-0.
Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic, akibebwa na daktari wa timu hiyo, Cosmas Kapinga.
![]() |
| Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage (MP), akimkabidhi jezi namba 8, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, aliyekuwa mgeni rasmi katika mpambano wa timu hizo. |




















No comments:
Post a Comment