TANGAZO


Saturday, April 28, 2012

Rais Kikwete awa mwenyeji mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha


 Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania,  Bernard Membe, mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), jijini Arusha leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), utakaofanyika mjini Arusha leo, tarehe 28 Aprili, 2012. (Picha zote na Ikulu)


 Rais Kibaki, akifurahia burudani ya ngoma ya Mganda ya wenyeji wa Ruvuma, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa KIA, jijini Arusha.


Rais Kibaki wa Kenya, akiwa na wenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kulia) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta (kushoto), mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa  KIA, jijini Arusha.


Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samwel Sitta, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa KIA, jijini Arusaha leo, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaofanyika, tarehe 28 Aprili, 2012.


Mwenyeji wa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya hiyo, wakitia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo, Aprili 28, 2012,  Hoteli ya Ngordoto, jijini Arusha.


Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakionesha hati walizosaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo, Aprili 28, 2012 katika Hoteli ya Ngordoto jijini Arusha.


Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakikaribishwa chakula cha mchana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Richard Sezibera baada ya kupiga picha ya pamoja kufuatia kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika Hoteli ya Ngordoto jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment