Wachezaji Ramadhan Singano (14), Simon Msuva (12) na Atupele Green, wa Ngorongoro Stars, wakikimbia kushangilia goli la tatu la timu hiyo, wakati ilipocheza na timu ya Sudan katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Kwanza ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Ubingwa wa Afrika kwa Vijana wa chini ya Umri wa miaka 20, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Ramadhan Singano wa Ngorongoro Stars (14), akimtoka Faris Abdallah wa Sudan katika mchezo huo.
Wachezaji Atupele Green (kulia) wa Ngorongoro Stars na Mohammed Abdallah wa Sudan wakiwania mpira wa juu wakati wa mchezo huo, uliomalizika kwa Ngorongoro kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Mchezaji Ahmed Ibrahim wa Sudan, akiondoa mpira uliokuwa umedhibitiwa na Ramadhan Singano wa Ngorongoro Stars, katika mchezo huo.
Ramadhan Singano wa Ngorongoro Stars (katikati), akidhibitiwa na Sharafeldin (18) na Gaksa Ramadhan (9) wa Sudan.
Wachezaji wa Ngorongoro Stars na Sudan, kwa pamoja, wakiwaaga mashabiki, Uwanja wa Taifa, baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Wachezaji wa Ngorongoro Stars na Sudan, wakipiga picha ya pamoja, baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa timu ya Sudan, Azhari Osman, akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kumalizika mchezo huo. Kushoto ni Ofisa Habari wa Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura.
Kocha Mkuu wa timu ya Ngorongoro Stars, Kim Poulsen, akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kumalizika mchezo huo. Kushoto ni Ofisa Habari wa Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura.
No comments:
Post a Comment