TANGAZO


Saturday, April 7, 2012

Msiba wa msanii Kanumba nyumbani kwao Sinza

 Baadhi ya vijana waombolezaji wakiwa nje ya nyumba ya msanii wa maigizo, Steven Kanumba, mara baada ya kutolewa habari za msiba leo asubuhi. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Baadhi ya wadau wa mambo ya filam, wakiwa kwenye msiba huo, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.


Baadhi ya wasanii wa maigizo, wakiwa wamejinamia kwa majonzi ya msanii mwenzao, Steven Kanumba, nyumbni kwao leo mchana.                



 Baadhi ya wasanii na watu mbalimbali waliofika kwenye msiba huo, nyumbani kwa marehemu msanii mwenzao, Steven Kanumba, Sinza Vatican, wakiwa wamejawa na huzuni kubwa kutokana na kumpoteza mwenzao huyo, usiku wa kuamkia leo.


Mkurugenzi wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta), Asha Baraka, akiwa pamoja na Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Kisangi, kwenye msiba huo.


 Waombolezaji, ndugu, jamaa na marafiki wa kiwa nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican leo mchana.


Kamati ya kushughulikia msiba wa Msanii wa Maigizo, marehemu Steven Kanumba, ikiwa katika kikao cha maandalizi ya msiba huo, nyumbani kwake Vatican Sinza, jijini Dar es Salaam.


 Mmoja wa wasanii wa maigizo, Salwa Badi 'Anitha', akisaidiwa na wasamaria wema baada ya kudondoka na kuzimia alipofika kwenye msiba huo, nyumbani kwa marehemu Kanumba leo. 


 Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan, akisaini kitabu cha maombolezo, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican leo mchana.


 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, akiwa na Mbunge wa Viti Maalum, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.


 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisaini kitabu cha maombolezo, nyumbani kwa marehemu, Steven Kanumba, alipofika nyumbani hapo kuwafariji wafiwa.


 Mbunge Idd Azzan, akizungumza na waandishi wa habari, alipofika kwenye msiba huo, nyumbani kwa marehemu, Sinza Vatican leo mchana.


 Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlacha, akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba huo.

 
 Mkurugenzi wa Utamaduni wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Hamans Mwansoko, akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo kwenye msiba huo.


 Vijana na baadhi ya mashabiki wa marehemu Kanumba, wakiwa wamepanda juu ya ukuta ili kushuhudia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka kwenye msiba huo, leo asubuhi.


Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ridhwan Kikwete (katikati), akijadili jambo pamoja na Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Wanatwanga Pepeta', Asha Baraka (kulia) Steven Nyerere (kushoto), kwenye msiba huo.

 Baadhi ya wasanii wa maigizo, ambao baadhi yao walicheza michezo pamoja na marehemu Kanumba wakiwa kwenye msiba huo, leo mchana.


 Vijana wakisubiri, kuangalia bahati zao ya kuweza kuingia kwenye nyumba yenye msiba huo, Sinza Vatican.


 Askari Polisi wakijaribu kudhibiti hali ya fujo kwa vijana na mashabiki wa msanii huyo, waliotaka kujaribu kuingia kwa nguvu kwenye nyumba hiyo.


 Vijana wakiwa nje ya geti la nyumba yenye msiba, Sinza Vatican, wakiwania kuingia kwenye nyumba hiyo.


Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye msiba huo, leo mchana.


 Mdogo wa marehemu Steven Kanumba, Seti, akizungumza na waandishi wa habari kwenye msiba huo leomchana.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye (kulia)kizungumza na waandishi wa habari, kwenye msiba huo, Sinza Vatican leo. Kushoto ni mshika fedha wa Chama hicho, Mwigulu Nchemba.



Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ridhwan Kikwete, akipeana mkono na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye (kulia), kwenye msiba huo, Sinza Vatican jana. Katikati ni Waziri wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta. 

No comments:

Post a Comment