Baadhi ya wageni, ndugu na jamaa wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee wakati wa kuaga mwili huo.
Kamanda wa Polisi mstaafu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, akiwasili kwenye viwanja hivyo, akilakiwa na Ofisa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, kikosi cha Usalama barabarani, Nadia Mohammed Said.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema (kushoto), akisindikizwa kupelekwa kwenye sehemu yake, wakati alipowasili viwanjani hapo jana.
Ofisa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, kikosi cha Usalama barabarani, Nadia Mohammed Said, akimfunga kitambaa cheusi kwa ajili ya kuomboleza mmoja wa Maofisa waongoza misafara wa kikosi hicho, alipowasili na pikipiki yake viwanjani hapo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, akisindikizwa kuchukua nafasi yake wakati alipowasili viwanjani hapo, wakati wa kuuaga mwili huo.
Bendi ya kikosi cha Jeshi la Polisi, ikitumbuiza katika hafla hiyo, viwanjani hapo.
Gari lililokuwa limebeba mwili wa marehemu IGP, mstaafu, marehemu Harun Mahundi, likiwasili kwenye viwanja vya Karimjee jana.
Jenenza lenye mwili wa marehemu IGP, mstaafu Harun Mahundi, likiteremshwa kwenye gari.
Maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi, wakilibeba jenenza lililokuwa na mwili wa marehemu IGP, mstaafu Harun Mahundi.
Baadhi ya wanafamilia ya IGP mstaafu, marehemu Harun Mahundi wakiwa kwenye viwanja hivyo tayari kuuaga mwili wake jana.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia), akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, katika hafla hiyo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda, akiwa na Jaji Mkuu, Othman Chande, Mwenyekiti wa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba pamoja na IGP, Said Mwema, wakiwa kwenye viwanja hivyo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda, akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi, Kingunge Ngombale Mwiru, akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakitoa heshima za mwisho kwa mwili huo.
Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu IGP, mstaafu Harun Mahundi, likiondolewa kwenye viwanja hivyo baada ya kumalizika kwa shughuli za kuaga jana.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waki, wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili huo, nyumbani kwa marehemu Harun Mahundi kabla ya kupelekwa makaburi ya Kinondoni kwa mazishi jana.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akiwa na mkewe, Mama Siti Mwinyi, IGP Said Mwema pamoja na Sir George Kahama wakiwa kwenye makaburi ya Kinondoni wakati wa mazishi ya marehemu IGP mstaafu Harun Mahundi jana. (Picha na Khamisi Mussa)
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akitoa wasifu wa marehemu IGP mstaafu Harun Mahundi wakati wa mazishi yake kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam jana. |
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akiweka mchanga kwenye kaburi hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Nahodha, akiweka mchanga kwenye kaburi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Said Mwema, akiweka mchanga kwenye kaburi hilo.
Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akisaidiwa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Mkuu wa Jeshi la Polisi wa zamani, Inspekta Jenerali mstaafu, marehemu Haruni Mahundi katika shughuli ya mazishi iliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. Kushoto ni mke wa Mwinyi, Mama Siti.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, Omar Mahita (kushoto) akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mahundi.
No comments:
Post a Comment