TANGAZO


Sunday, April 1, 2012

Mancini asema Man United itateleza pia

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini, ameonesha matumaini mahasimu wao Manchester United watapoteza pointi katika mbio zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu.
Roberto Mancini anatumai Man United watateleza
Roberto Mancini anatumai Man United watateleza
Baada ya Manchester City kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Sunderland, Manchester United iwapo itailaza Blackburn siku ya Jumatatu itaiacha nyuma City kwa pointi tano.
"Nadhani Jumatatu Manchester United huenda nao watatoa sare," alisema Mancini. "Katika michezo minane inawezekana kutoka sare miwili. United inaweza kukabiliwa na wakati mgumu.
Matokeo dhidi ya Sunderland yameibakiza Manchester City nafasi ya pili ikiwa na pointi 71 na michezo saba kibindoni, wakati Manchester United inaongoza kwa kujikusanyia pointi 73 na imebakisha michezo minane.
Lakini Man United imeweza kushinda michezo miwili tu kati ya safari zake nane za michezo ya ligi kwenye uwanja wa Ewood Park na Mancini ametabiri watateleza kwa mara nyingine.
Mancini ameelezea mechi dhidi ya Sunderland ilikuwa "pambano gumu, lililojaa msisimko " baada ya Man City kuwa nyuma kwa mabao 3-1 na walipigana kiume na kujipatia angalao pointi moja.
"Nadhani yalikuwa matokeo sahihi, kutoka sare, lakini hatukucheza vizuri," Mancini alilalama.
"Nilifurahia dakika 10 za mwisho, kwa dakika nyingine 80 sikuwa na furaha kwa sababu hatukucheza vizuri sana. Sijui kwa nini.
Akizungumzia safari yao ya siku ya Jumapili ijayo kuikabili Arsenal katika uwanja wa Emirates, Mancini amesema: "Nina hakika tutafanya vizuri kuliko mechi ya Sunderland.
"Hatukuwa na mshambuliaji wetu Aguero na kwa sababu hiyo nimevunjika moyo. Natumai atakuwa amepona kwa mtanange ujao.''
Meneja wa Sunderland Martin O'Neill amesema kuna nafasi nyingi katika mbio za kuwania ubingwa.
"City ina kikosi chenye ubora wa hali ya juu," alisema.
"Kutakuwa na heka heka za hapa na pale kabla msimu haujamalizika na Manchester United watakabiliana nasi kwetu katika mechi ya mwisho kumalizia msimu."

No comments:

Post a Comment