TANGAZO


Thursday, April 19, 2012

Kapteni ana mimba

Kapteni wa Uingereza Faye White ana mimba
Kukiwa kumesalia siku mia moja kwa michezo ya Olimpiki kuanza mjini London ,Kapteni wa timu ya Soka ya Uingereza kwa akina dada Bi Faye White hatacheza katika mashindano hayo.
Bi White hataichezea timu yake ya taifa wakati wa Olimpiki kwa sababu ana mimba.
Bibi huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye nyumbani anachezea timu ya akina dada ya Arsenal amesema anatarajia kujifungua mwezi wa Oktoba.
Bi White amedokeza kuwa huenda pia akajiuzulu kutoka timu hiyo ya taifa mara tu baada ya kujifungua
" Nina mimba na kwa mara ya kwanza kufikia mwezi wa Oktoba nitakuwa mama” aliiambia BBC.
Kapteni huyu atakumbukwa kwamba wakati wa robo fainali ya kombe la dunia kwa akina dada mwaka wa 2011 walipochuana na Ufaransa alikosa mkwaju wa penaliti.
Bi White anasema hana uhakika kama baada ya kujifungua ataendelea kuchezea klabu yake ya Arsenal au atastaafu kabisa kutoka mchezo huo.

No comments:

Post a Comment