TANGAZO


Saturday, April 14, 2012

Iran yazungumza mradi wake wa nuklia

Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya mwaka mmoja, Iran inakutana na wawakilishi wa mataifa makubwa kujadili mpango wake wa nuklia.
Rais Ahmedinajad wa Iran akikagua zana za nuklia
Rais Obama amesema mkutano huo ni fursa ya mwisho ya kutafuta ufumbuzi kwa njia za kidiplomasia.
Iran inakanusha kuwa inajaribu kutengeneza silaha za nuklia, lakini kuna tetesi kuwa Israil pengine inajitayarisha kushambulia vituo vya nuklia vya Iran.
Wapatanishi wa Iran wanakutana na wajumbe wa Marekani, Urussi, Uchina, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani mjini Istanbul, Uturuki.
Wanadiplomasia wanasema kuanza tena mazungumzo ni uzuri, lakini hayakuelekea kuwa yataleta mafanikio makubwa.

No comments:

Post a Comment