TANGAZO


Saturday, April 14, 2012

Baraza lakubaliana kuhusu Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kutuma ujumbe wa mwanzo kwenda Syria, kusimamia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza Alkhamisi.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likijadili Syria
Baraza hilo piya limelaani ukiukaji wa haki za kibinaadamu unaofanywa na wanajeshi wa Syria, na maovu yanayofanywa na yale yaliyoitwa makundi yenye silaha.
Lakini wakati baraza hilo lilipoanza kikao, makubaliano ya kusitisha mapigano yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, yalikuwa yanaonekana karibu kuvunjika.
Inaarifiwa wanajeshi wa serikali wamepiga mizinga mitaa miwili ya mji wa Homs, wa tatu kwa ukubwa.
Wanaharakati wanasema watu 17 waliuwawa.
Piya kuna taarifa kuwa watu kadha walipigwa risasi na kuuwawa kwenye mazishi katika mji wa Aleppo, kaskazini mwa nchi, wakati wanajeshi walipofyatua risasi.
Televisheni ya taifa imewalaumu waasi kuwa walifanya hayo.

No comments:

Post a Comment